Monday, July 31, 2017

ISAYA MSANGI AWASHA MOTO MKALI SANA MWANZA... TAZAMA HAPA...



Mwimbaji wa Nyimbo za injili Nchini Tanzania Isaya Msangi, amefanya kufuru katika ibada za Jumapili alizokaribishwa kuhudumu huko Jijini Mwanza katika kanisa la Ukombozi na kuwafanya waumini kupagawa kwa nyimbo zake mbili mpya alizoimba.

Akizungumza na Gospel 1 Magazine Isaya Msangi Ambaye pia ni daktari wa maginjwa ya binaadamu, amesema kuwa hakutegemea mapokeo ya kiasi hicho kwani nyimbo hizo ni mpya na hazina promo bado, lakini ameshangazwa na jinsi watu walivyozipokea nyimbo hizo kwani watu hawakutaka hata kukaa chini.

"... hakika nimeuona mkono wa Mungu katika ujio wa Nyimbo zangu hizi imbili ambazo nilikuwa bado sijazitambulisha rasmi, lakini kwa moto ulivyowaka pale Mwanza kusema ukweli, mkono wa Mungu uko juu yangu... naamini kabisa nyimbo hizi zitakuja kuwa kuja moto wa kuotea mbali..."

Isaya amewasha moto huo katika kanisa la Ukombozi chini ya Mchungaji BG Malisa Jijini Mwanza - Tanzania ambapo aliimba nyimbo zake mpya Kimeeleweka na Leo ni Zamu Yako.

TAZAMA VIDEO HAPA

Wednesday, July 26, 2017

EBENEZA WIMBO WA MWAKA... NI CHANGAMOTO KWA WAIMBAJI WA INJILI...



Muimbaji wa wa Kitambo na Producer wa Kitambo na Kijana mwenye vipaiji vingi, wenyewe wanasema Muhenga, Mussa Sikabwe, ametangaza kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la EBENEZA, Ukiwa ni wimbo uliotengenezwa na kuimbwa katika viwango vingine.

Akizungumza na Gospel 1 MagazineMussa Sikabwe maarufu kwa Jina la MO, amesema kuwa ameamua kuachia wimbo huo ikiwa kama ni utambulisho wake rasmi katika Tasnia ya nyimbo za Injili, kwani hapo nyuma ni kweli alikuwa anaimba Gospel lakini alikuwa bado hajaingia kabisa.

"... unajua kila kitu ni wito, na hii kazi yaMungu tunafanya kulingana na Wito... kila mtu kanisani ameitwa kwa Karama yake, kun walioitwa kwa Uchungaji wapo walioitwa kwa ushemasi, Uinjilisti na vipawa vingine vingi, lakini mimi ni meitwa kwa Uimbaji, lakini bado muda wangu ulikuwa haujafika... alisema Mussa.

"... sio kuwa nilikuwa siimbi kabisa hapana, hata ukiingia you tube utakuta nyimbo yangu nyingine, lakini nasema tu muda wangu ulikuwa haujatimia, lakini kwa sasa ninaamini kuwa Mungu sasa ameniruhusu nianze Rasmi na ndio maana nimeamua nianze na Wimbo huu uitwao EBENEZA. ameendelea kusema Mussa

Mussa amesema kuwa pamoja na Ebeneza kwa sasa ana nyimbo nyingine tatu, ambapo mmpja alishauweka you tube tayari unaitwa DAMU SUKUMA MOYO, lakini pia yuko mbioni kukamilisha nyimbo zilizobaki zitakazo kuwa ndani ya Album ya Ebeneza.

amesema kuwa hivi karibuni atatoa kwanza video ya wimbo huu wa Ebeneza wakati akiwa anaendelea kumalizia audio zilizobaki katika albabu yake.

Mussa Sikabwe amesema kuwa yeye yuko tayari kwa huduma mbalimbali kwani kazi anayoifanya sio ya kwake bali ya Mungu aliye mtuma... unampata kwa no. 0674 411 705 - 0784 130 176

KUSIKILIZA WIMBO WA ENEZA, HUU HAPA

Thursday, December 8, 2016

BEATRICE KITAULI ATAMANI KUIVUSHA MIPAKA VIDEO YA KESHO...



Mwimbaji wa nyimbi za injili ambaye anakuja juu na anayenaongoza kwa nyimbo zake zenye tungo kali, Beatrice Kitauli, ameitambulisha rasmi video ya wimbo wake mpya alioimba kwa kushirikiana na Malkia wa Gospel nchini Tanzania, Rose Muhando.

Akiongea na meza ya Jicho Wazi ambao ni mtandao dada wa MO Design, Beatrice kitauli amesema Video tayari iko kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, lakini pia anatarajia kuisambaza kwenye vituo mbalimbali vyatelevisheni vya hapa nchini ikiwa ni pamoja na vile vya nchi za nje.
.
" Video iko tayari youtube na kwenye mitandao mingine ya kijamii, lakini pia nafikiria jinsi ya kuipeleka mbele zaidi nikimaanisha vituo vya televisheni vya nje yaTanzania ikiwezekana hata Trece Tv..." Alisema Beatrice Kitauli.

VIDEO HII HAPA...

MZEE WA UPAKO AENDELEA KUJIKOSHA KWA KUDONOADONOA...


DAR ES SALAAM: Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake ameendelea kujibu madai hayo kwa mtindo wa ‘kudonoa donoa’ na jana aliwataka wanaodai kuwa alilewa siku hiyo wataje alikunywa pombe gani na katika baa gani. 
Wiki mbili zilizopita, taarifa kwenye vyombo vya habari zilisema kwamba Mchungaji Lusekelo alikwaruzana na majirani zake huku akidaiwa kuwa alikuwa amelewa jambo ambalo lilifanya achukuliwe na kuhojiwa na polisi.
Lakini, tangu kuibuka kwa tukio hilo alikataa kulitolea ufafanuzi licha ya kutafutwa na vyombo vya habari, hata pale alipohudhuria ibada kanisani kwake aliwaambia waumini wake hatalizungumzia na badala yake alidonoadonoa baadhi ya matukio.
Alipokwenda kanisa kwake kwa mara ya kwanza Novemba 25, Mchungaji Lusekelo alisema; “Kuna kitu nilikuwa nataka nikiseme, lakini sitakisema ili waendelee kusema haohao waliokuwa wanasema.Wakawaulize wenyewe. Nimeyaona magazeti hapa, ooh Mzee wa Upako, ooh Mzee wa Upako, sisemi. Sasa leo yupo hapa, na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”
Lakini, Novemba 28, Mchungaji huyo akajibu baadhi ya hoja akisema kwanza, maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye Biblia. Pili, watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.
 Hoja nyingine alisema watu hao hawakuwa jirani zake kama inavyodaiwa kwani mtaani kwake wanaishi kama majambazi kutokana na mazingira ya kutofahamiana.
Jana, Mchungaji Lusekelo akiwahubiria waumini wake alidonoa tena eneo jingine linalohusiana na tukio hilo, kwamba wanaodai alikuwa amelewa pombe, waeleze alikunywa pombe gani na baa gani.
Akikaribishwa kwa wimbo wa kuabudu uitwao, ‘Nina haja nawe’ kabla ya kuanza kumtunza kwa sadaka, Mchungaji Lusekelo alisema watu wanaotuhumu kuwa alilewa, wanatakiwa kueleza alikunywa pombe gani na alikunywa akiwa eneo gani.
“Wiki iliyopita nilikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani, baadhi ya maofisa wakaniona , wewe Mzee wa Upako… Mzee wa Upako, askari mmoja akaniuliza wewe Mzee wa Upako unachukua sadaka halafu unaenda kunywa pombe. Nikawauliza, hiyo pombe nilikunywa wapi, halafu pombe zipo za aina nyingi, taja ni pombe gani, ukienda mbali zaidi ungeuliza nililewa nini, maana hata upako wa roho mtakatifu ni ulevi,” alisema.
“Lakini kuna majina ya watu, mitaani inaitwa pombe, sasa sijui ni pombe gani hiyo….watashindana sana. Lakini kushindana siyo tatizo, je, mtashinda? Eti oooh hayo maneno tu hata kwenye kanga yapo, subiri tusiandikie mate na wino upo, ukitaka kummaliza Mzee wa Upako we mpige risasi tu,” alisema huku akishangiliwa na waumini wake.
 Alisema hakuna mwanadamu atakayeweza kumwangusha kwa kipawa na kalama Mungu aliyompatia.
“Ndiyo maana unapojiita mtume leo unakuwa unajirusha kwenye harakati ambazo zilijengwa na baba zetu, ndiyo maana kumshinda shetani ni lazima, kuna mfumo umejengwa na mfumo huu uko imara kama chuma cha pua,” alisema.
Katika ibada ya wiki iliyopita, mchungaji huyo alisema taarifa zinazosambazwa kumchafua hazitamvunja moyo wa kuendelea kufanya kazi ya uchungaji, huku akihoji kwanini magazeti yanaandika mabaya pekee na hayaandiki habari za uponyaji anaofanya kanisani kwake.

Monday, August 22, 2016

VIDEO YA MAUA YA KWAKE BEATRICE KITAULI IKO HAPA...


Beatrice H Kitauli

Muimbaji wa nyimbo za injili Beatrice Kitauli ameitambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao MAUA.
Wimbo huo ni ule unaobeba Album yake iitwayo Mau. akizungumza na MO Design Beatrice amesema kuwa ameamua kuachi wimbo huo mmoja kwanza ili kuwaweka watu tayari kwa ajili ya album yake hiyo ijayo.

" sio kwamba nimefanya video ya wimbo huo mmoja tu, la hasha nafanya album nzima ila nimeamua kuachia huo mmoja kwanza ili watu waone ubora wa kile kitu nilichokuwa nawaambia watu kuwa na kifanya"... alisema Beatrice.

Beatrice ni muimbaji mpya katika tasnia ya uimbaji wa nyimbo za injili, lakini pia ni mmoja kati ya up coming wanaofanya vizuri katika mwaka huu wa  2016,
ukiuzungumzia wimbo wa MAUA ni wimbo ambao unaendelea kushika chart za juu katika media tofauti nchini ikiwemo na mitandao ya kijamii.

VIDEO HII HAPA

Wednesday, July 13, 2016

IKO HAPA SABABU YA ASKOFU GWAJIMA KUKAMATWA NA POLISI UWANJA WA NDEGE DAR...


Gwajima
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima jana July 12 2016 amekamatwa na polisi wakati anawasili Tanzania kutokea ughaibuni ambapo baada ya kukamatwa alichukuliwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kituoni.
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema Gwajima amehojiwa kutokana na kauli yake ya uchochezi aliyoitoa kabla hajasafiri kwenda nje ya nchi. kamanda sirro amesema kuwa tayari walishamuhoji na upelelezi unaendelea.
Alipofika tu uwanja wa ndege alichukuliwa, yeye alifikiri anaweza tu kuja kimyakimya bila kuonekana…. uwezekano wa kutoonekana ni mdogo sana, tumeshamuhoji vizuri upelelezi unaendelea na tukipata ushahidi wa kutosha sheria itachukua mkondo wake, yuko nje kwa dhamana‘ – alisema Sirro.

Saturday, July 9, 2016

BEATRICE KITAULI WA MAUA ANG'ATWA NA NYOKA AKIWA LOCATION...




Hakuna kazi Duniani ambayo Binadamu yeyote anaweza kuifanya ikakosa changamoto, lakini pia unaambiwa ukiona changamoto zimekuwa nyingi ujue mafanikio yanakaribia.
Muimbaji wa nyimbo za injili na ambaye anatamba na kibao cha MAUA, Beatrice Kitauli, aling'atwa na nyoka akiwa katika ukaguzi wa Location kwa ajili ya shooting ya wimbo wa MAUA.
Akiongea na mtandoa pacha wa mtandao huu, (JICHO WAZI), Beatrice amesema kuwa nyoka huyo aliibuka ghafla na kumng'ata mguuni, lakini aliwahi kupatiwa huduma za haraka zilizozuia sumu kusambaa na sasa anaendelea vizuri.

Beatice amewaomba Mashabiki wake wasiwe na hofu kwani anaendelea vizuri na kazi ya kuhakikisha Video ya Album ya MAUA inakamilika kwa msaada wa Mungu, lakini pia ameomba msaada wa maombi kwani bila maombi hawezi kufanikisha.
Mitandao ya MO Designtz, Jicho Wazi na Soka Sport Inakupa pole sana Beatrice na Mungu awe nawe ili ukamilishe Kazi zako salama.