
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania Beatrice Kitauli ambaye anatamba sasa na Kibao kiitwacho MAUA, amesema sasa ni zamu yake kwani Album aliyoiandaa ni moto wa kuotea mbali.
akiongea kwa njia ya mtandao na mwandishi wa habari hizi, Beatrice amewatahadharisha wakongwe kwenye tasnia hii ya uimbaji wa nyimbo za injili kukaa chonjo kwani albumu ya MAUA itapiku album nyingi za wakongwe ambao wameonekana kulegalega katika uimbaji kwa wakati huu.
"... hii ni kazi ya Mungu tunayofanya lakini pia tunatakiwa kutumia vizuri vipaji tulivyopewa ili kuufikisha ujumbe kwa walengwa ukiwa katika hali nzuri, kusema kweli Album hii ya MAUA, sijisifii lakini nasema baadhi ya wakongwe wajihadhari kwani moto wa Album hii sio wa Kitoto..." alisema Beatrice.

Beatrice amesemakuwa Video ya Album hiyo ndio iko jikoni inatengenezwa chini ya kambuni iitwayo kwetu studio ambapo album hiyo inabeba jumla ya nyimbo Nane. ikiwa ni pamoja na 1. Maua, 2. Roho Yangu 3. Ole Wako 4. Acha Kuloga 5.Shamesha Vavae 6. Yupo Mungu 7. Niseme na Yesu na wa 8. Maua no.2
"... Kusema ukweli nawaomba watanzania watarajie kupata Video bora ambazo ni tofauti na zile zilizozoeleka, hizi zitakuwa nzuri na zinazoendana na Ujumbe wa nyimbo husika..." alimalizia Beatrice.
akasema pia kwa yeyote anayetaka kuupata wimbo wa Maua kupitia Whatsap anaweza kutumia namba hii kuupata. 0757 890 451
No comments:
Post a Comment