Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli amemshukuru nabii TB Joshua wa Nigeria kwa msaada alioutoa kwa Tanzania baada ya kuongea nae na kumueleza maono yake ya kusaidia wazee na watu wenye ulemavu..
Mama Janeth amesema ‘Namshukuru kwa msaada huu mkubwa aliotuwezesha katika kambi hii ya Wazee, nilipoongea nae nilimueleza maono yangu kwa ajili ya huduma hii ninayofanya ya kuhudumia Wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza‘
‘Niliongea nae akasema ataniunga mkono na kama mnavyoona hapa leo yeye mwenyewe ametuma mwakilishi wake amenunua vyakula, namshukuru Nabii TB Joshua kwa kutoa, amekua akitoa misaada bila kujali itikadi za dini wala nchi… Mungu ambariki sana‘ Aliongea Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
No comments:
Post a Comment