
Benard Peter Mwinje
Mwimbaji wa nyimbo za injili na Mwalimu wa Kwaya Benard Peter Mwinje ameliambia Jicho Wazi kuwa tayari amekamilisha kupika Album yake yenye jumla ya nyibi Nane( 8)Album hiyo iliyobeba jina la CHANZO CHA MATEZO, itaanza kupatikana mitaani hivi karibuni kwani kila kitu kiko tayari.
"... kusema kweli namshukuru Mungu kwani nimemaliza Kuandaa album yangu ambayo ina kwenda kwa jina la Chanzo cha mateso, wengi walidhani ntafeli lakini kwauwezo wa Mungu nimemaliza na hivi karibuni ntaaza kuisambaza kwani kama unavyoona hii hapa ndio kava lake ambalo nimetengeneza na Kampuni ya MO Design..." Alisema Mwinje.
akaongeza kuwa ataanza kuuza Audio tu peke yake ili apate pesa ya kuongezea katika maandalizi aliyonayo ya kufanya Video. Mwinje pia aliweka wazi kuwa yuko tayari kupokea mialiko mbalimbali kwani anachokifanya ni huduma ambayo iko ndani yake na kazi ambayo ametumwa na Mungu wake.
Nyimbo ambazo zinpo katika Album hii ya Chanzo Cha Mateso ni pamoja na. Chanza cha Mateso, Ukiwa na Raha, Mbinguni, Dhahabu, Duniani, Kwa neema, Nijifiche wapi pamoja na Mungu Wangu.
No comments:
Post a Comment