
Nyota Njema huonekana asubuhi, huu ni usemi wa kiswahili ambao watu wengi huutumia kama metrhali kama mimi pianinavyoutumia kuuzungumzia wimbo wa Maua wa kwake Beatrice Kitauli.
Wimbo huu ni wimbo ambao unatamba katika masikio ya watu kwa sasa kupitia vituo mbalimbali vya Radio hapa nchini na kwenye mitandao mingi ya Kijamii.
naweza kusema katika nyimbo bora ambazo zimekwisha kutoka katika mwaka huu, wimbo huu wa Maua unaweza kuchukua nafasi ya kwanza kwa uboza.
tunapozungumzia ubora tunamaanisha kuwa ni wimbo mzuri amboa unaongoza kupendwa na watu.
Wimbo huu sasa unaweza kuupata kama ring tone kwa kutuma ujumbe 2131032 kwenda 15050 Tigo Beat. kama ilivyoelekeza kweny picha hapo juu

Wimbo huu wa maua utapatikana pia katika Album ya MAUA ya kwake Beatrice Kitauli itayo kuwa mitaani hivi karibu. kinachosubiriwa ili album hii iingie mitaani ni video ambayo iko jikoni inaandaliwa chini ya kampuni ijulikanayo kama Kwetu Studio.
Beatrice anasisitiza kuwa video zitakuwa na kiwango cha hali ya juu na ambacho kitawafurahisha watazamaji wote.
No comments:
Post a Comment