
Mwimbaji wa nyimbi za injili ambaye anakuja juu na anayenaongoza kwa nyimbo zake zenye tungo kali, Beatrice Kitauli, ameitambulisha rasmi video ya wimbo wake mpya alioimba kwa kushirikiana na Malkia wa Gospel nchini Tanzania, Rose Muhando.
Akiongea na meza ya Jicho Wazi ambao ni mtandao dada wa MO Design, Beatrice kitauli amesema Video tayari iko kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, lakini pia anatarajia kuisambaza kwenye vituo mbalimbali vyatelevisheni vya hapa nchini ikiwa ni pamoja na vile vya nchi za nje.
.
" Video iko tayari youtube na kwenye mitandao mingine ya kijamii, lakini pia nafikiria jinsi ya kuipeleka mbele zaidi nikimaanisha vituo vya televisheni vya nje yaTanzania ikiwezekana hata Trece Tv..." Alisema Beatrice Kitauli.
VIDEO HII HAPA...
No comments:
Post a Comment