Thursday, December 8, 2016

BEATRICE KITAULI ATAMANI KUIVUSHA MIPAKA VIDEO YA KESHO...



Mwimbaji wa nyimbi za injili ambaye anakuja juu na anayenaongoza kwa nyimbo zake zenye tungo kali, Beatrice Kitauli, ameitambulisha rasmi video ya wimbo wake mpya alioimba kwa kushirikiana na Malkia wa Gospel nchini Tanzania, Rose Muhando.

Akiongea na meza ya Jicho Wazi ambao ni mtandao dada wa MO Design, Beatrice kitauli amesema Video tayari iko kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, lakini pia anatarajia kuisambaza kwenye vituo mbalimbali vyatelevisheni vya hapa nchini ikiwa ni pamoja na vile vya nchi za nje.
.
" Video iko tayari youtube na kwenye mitandao mingine ya kijamii, lakini pia nafikiria jinsi ya kuipeleka mbele zaidi nikimaanisha vituo vya televisheni vya nje yaTanzania ikiwezekana hata Trece Tv..." Alisema Beatrice Kitauli.

VIDEO HII HAPA...

MZEE WA UPAKO AENDELEA KUJIKOSHA KWA KUDONOADONOA...


DAR ES SALAAM: Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake ameendelea kujibu madai hayo kwa mtindo wa ‘kudonoa donoa’ na jana aliwataka wanaodai kuwa alilewa siku hiyo wataje alikunywa pombe gani na katika baa gani. 
Wiki mbili zilizopita, taarifa kwenye vyombo vya habari zilisema kwamba Mchungaji Lusekelo alikwaruzana na majirani zake huku akidaiwa kuwa alikuwa amelewa jambo ambalo lilifanya achukuliwe na kuhojiwa na polisi.
Lakini, tangu kuibuka kwa tukio hilo alikataa kulitolea ufafanuzi licha ya kutafutwa na vyombo vya habari, hata pale alipohudhuria ibada kanisani kwake aliwaambia waumini wake hatalizungumzia na badala yake alidonoadonoa baadhi ya matukio.
Alipokwenda kanisa kwake kwa mara ya kwanza Novemba 25, Mchungaji Lusekelo alisema; “Kuna kitu nilikuwa nataka nikiseme, lakini sitakisema ili waendelee kusema haohao waliokuwa wanasema.Wakawaulize wenyewe. Nimeyaona magazeti hapa, ooh Mzee wa Upako, ooh Mzee wa Upako, sisemi. Sasa leo yupo hapa, na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”
Lakini, Novemba 28, Mchungaji huyo akajibu baadhi ya hoja akisema kwanza, maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye Biblia. Pili, watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.
 Hoja nyingine alisema watu hao hawakuwa jirani zake kama inavyodaiwa kwani mtaani kwake wanaishi kama majambazi kutokana na mazingira ya kutofahamiana.
Jana, Mchungaji Lusekelo akiwahubiria waumini wake alidonoa tena eneo jingine linalohusiana na tukio hilo, kwamba wanaodai alikuwa amelewa pombe, waeleze alikunywa pombe gani na baa gani.
Akikaribishwa kwa wimbo wa kuabudu uitwao, ‘Nina haja nawe’ kabla ya kuanza kumtunza kwa sadaka, Mchungaji Lusekelo alisema watu wanaotuhumu kuwa alilewa, wanatakiwa kueleza alikunywa pombe gani na alikunywa akiwa eneo gani.
“Wiki iliyopita nilikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani, baadhi ya maofisa wakaniona , wewe Mzee wa Upako… Mzee wa Upako, askari mmoja akaniuliza wewe Mzee wa Upako unachukua sadaka halafu unaenda kunywa pombe. Nikawauliza, hiyo pombe nilikunywa wapi, halafu pombe zipo za aina nyingi, taja ni pombe gani, ukienda mbali zaidi ungeuliza nililewa nini, maana hata upako wa roho mtakatifu ni ulevi,” alisema.
“Lakini kuna majina ya watu, mitaani inaitwa pombe, sasa sijui ni pombe gani hiyo….watashindana sana. Lakini kushindana siyo tatizo, je, mtashinda? Eti oooh hayo maneno tu hata kwenye kanga yapo, subiri tusiandikie mate na wino upo, ukitaka kummaliza Mzee wa Upako we mpige risasi tu,” alisema huku akishangiliwa na waumini wake.
 Alisema hakuna mwanadamu atakayeweza kumwangusha kwa kipawa na kalama Mungu aliyompatia.
“Ndiyo maana unapojiita mtume leo unakuwa unajirusha kwenye harakati ambazo zilijengwa na baba zetu, ndiyo maana kumshinda shetani ni lazima, kuna mfumo umejengwa na mfumo huu uko imara kama chuma cha pua,” alisema.
Katika ibada ya wiki iliyopita, mchungaji huyo alisema taarifa zinazosambazwa kumchafua hazitamvunja moyo wa kuendelea kufanya kazi ya uchungaji, huku akihoji kwanini magazeti yanaandika mabaya pekee na hayaandiki habari za uponyaji anaofanya kanisani kwake.

Monday, August 22, 2016

VIDEO YA MAUA YA KWAKE BEATRICE KITAULI IKO HAPA...


Beatrice H Kitauli

Muimbaji wa nyimbo za injili Beatrice Kitauli ameitambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao MAUA.
Wimbo huo ni ule unaobeba Album yake iitwayo Mau. akizungumza na MO Design Beatrice amesema kuwa ameamua kuachi wimbo huo mmoja kwanza ili kuwaweka watu tayari kwa ajili ya album yake hiyo ijayo.

" sio kwamba nimefanya video ya wimbo huo mmoja tu, la hasha nafanya album nzima ila nimeamua kuachia huo mmoja kwanza ili watu waone ubora wa kile kitu nilichokuwa nawaambia watu kuwa na kifanya"... alisema Beatrice.

Beatrice ni muimbaji mpya katika tasnia ya uimbaji wa nyimbo za injili, lakini pia ni mmoja kati ya up coming wanaofanya vizuri katika mwaka huu wa  2016,
ukiuzungumzia wimbo wa MAUA ni wimbo ambao unaendelea kushika chart za juu katika media tofauti nchini ikiwemo na mitandao ya kijamii.

VIDEO HII HAPA

Wednesday, July 13, 2016

IKO HAPA SABABU YA ASKOFU GWAJIMA KUKAMATWA NA POLISI UWANJA WA NDEGE DAR...


Gwajima
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima jana July 12 2016 amekamatwa na polisi wakati anawasili Tanzania kutokea ughaibuni ambapo baada ya kukamatwa alichukuliwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kituoni.
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema Gwajima amehojiwa kutokana na kauli yake ya uchochezi aliyoitoa kabla hajasafiri kwenda nje ya nchi. kamanda sirro amesema kuwa tayari walishamuhoji na upelelezi unaendelea.
Alipofika tu uwanja wa ndege alichukuliwa, yeye alifikiri anaweza tu kuja kimyakimya bila kuonekana…. uwezekano wa kutoonekana ni mdogo sana, tumeshamuhoji vizuri upelelezi unaendelea na tukipata ushahidi wa kutosha sheria itachukua mkondo wake, yuko nje kwa dhamana‘ – alisema Sirro.

Saturday, July 9, 2016

BEATRICE KITAULI WA MAUA ANG'ATWA NA NYOKA AKIWA LOCATION...




Hakuna kazi Duniani ambayo Binadamu yeyote anaweza kuifanya ikakosa changamoto, lakini pia unaambiwa ukiona changamoto zimekuwa nyingi ujue mafanikio yanakaribia.
Muimbaji wa nyimbo za injili na ambaye anatamba na kibao cha MAUA, Beatrice Kitauli, aling'atwa na nyoka akiwa katika ukaguzi wa Location kwa ajili ya shooting ya wimbo wa MAUA.
Akiongea na mtandoa pacha wa mtandao huu, (JICHO WAZI), Beatrice amesema kuwa nyoka huyo aliibuka ghafla na kumng'ata mguuni, lakini aliwahi kupatiwa huduma za haraka zilizozuia sumu kusambaa na sasa anaendelea vizuri.

Beatice amewaomba Mashabiki wake wasiwe na hofu kwani anaendelea vizuri na kazi ya kuhakikisha Video ya Album ya MAUA inakamilika kwa msaada wa Mungu, lakini pia ameomba msaada wa maombi kwani bila maombi hawezi kufanikisha.
Mitandao ya MO Designtz, Jicho Wazi na Soka Sport Inakupa pole sana Beatrice na Mungu awe nawe ili ukamilishe Kazi zako salama.

Tuesday, June 21, 2016

WIMBO WA MAUA WAZIDI KUNG'ARA... SASA UNAWEZA KUUPATA KAMA MWITO KWENYE SIMU...




Nyota Njema huonekana asubuhi, huu ni usemi wa kiswahili ambao watu wengi huutumia kama metrhali kama mimi pianinavyoutumia kuuzungumzia wimbo wa Maua wa kwake Beatrice Kitauli.
Wimbo huu ni wimbo ambao unatamba katika masikio ya watu kwa sasa kupitia vituo mbalimbali vya Radio hapa nchini na kwenye mitandao mingi ya Kijamii.
naweza kusema katika nyimbo bora ambazo zimekwisha kutoka katika mwaka huu, wimbo huu wa Maua unaweza kuchukua nafasi ya kwanza kwa uboza.
tunapozungumzia ubora tunamaanisha kuwa ni wimbo mzuri amboa unaongoza kupendwa na watu.
Wimbo huu sasa unaweza kuupata kama ring tone kwa kutuma ujumbe 2131032 kwenda 15050 Tigo Beat. kama ilivyoelekeza kweny picha hapo juu



Wimbo huu wa maua utapatikana pia katika Album ya MAUA ya kwake Beatrice Kitauli itayo kuwa mitaani hivi karibu. kinachosubiriwa ili album hii iingie mitaani ni video ambayo iko jikoni inaandaliwa chini ya kampuni ijulikanayo kama Kwetu Studio.
Beatrice anasisitiza kuwa video zitakuwa na kiwango cha hali ya juu na ambacho kitawafurahisha watazamaji wote.

Monday, June 13, 2016

ALBUM YA MAUA YAWA GUMZO HATA KABLA YA UJIO WAKE RASMI... WADAU WAFUNGUKA...



Katika hali isiyotarajiwa ujio wa Album ya  MAUA ya kwake Beatrice Kitauli, ambayo iko mbioni kuachiwa, imekuwa gumzo la jiji Kabla hata bado haijaachiwa na kuingia mitaani kwa wadau na wasikilizaji mbalimbai.
hali hii imetokana na wimbo unaobeba jina la Ulbum hiyo kuwafikia baadhi ya watu na kuona uzuri wa wimbo huo,

"... kusema kweli nilikuwa nikiona tu posti mbalimbali kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikizungumzia ujio wa Album hiyo, kama kunapost ile ya SMAGAZINE, nilipoiona nikakuta kuna namba ya muimbaji Beatrice ikabidi niingie whatsap nikamuomba wimbo huo, yaani ni mzuri..." akisema kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la boniface.
 
lakini yvonne yeye anasema aliusikia kupitia redioni lakini hakumbuki ilikuwa ni kituo gani cha redio.
"... wimbo wa maua naufahamu nilishausikia kupitia redio lakini sikumbuki ilikuwa redio gani, kusema ule ukweli wimbo ni mzuri tunasubiri tuone video..."
alisema Yvonne.
Video ya Album ya MAUA ya kwake Beatrice Kitauli iko jikoni na yeye mwenyewe anawaambia mashabiki wake kuwa wategemee video yenye ubora wa hali ya juu.
"... hii itakuwa ni video tofauti na zile ambazo watu walizoea kuziona, video na matukio yatakuwa yanaendana na ujumbe uliomo kwenye nyimbo, nataka watu wajiandae tu kuona kitu kipya ambacho hawajawahi kukiona..." alimalizia beatrice.
Album ya maua ilitengenezwa katika Studio za Eck Production chini ya Produce Eck.

Thursday, June 9, 2016

ALBUM YA MAUA YA KWAKE BEATRICE KITAULI IMEKUWA GUMZO LA JIJI...



Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania Beatrice Kitauli ambaye anatamba sasa na Kibao kiitwacho MAUA, amesema sasa ni zamu yake kwani Album aliyoiandaa ni moto wa kuotea mbali.
akiongea kwa njia ya mtandao na mwandishi wa habari hizi, Beatrice amewatahadharisha wakongwe kwenye tasnia hii ya uimbaji wa nyimbo za injili kukaa chonjo kwani albumu ya MAUA itapiku album nyingi za wakongwe ambao wameonekana kulegalega katika uimbaji kwa wakati huu.
"... hii ni kazi ya Mungu tunayofanya lakini pia tunatakiwa kutumia vizuri vipaji tulivyopewa ili kuufikisha ujumbe kwa walengwa ukiwa katika hali nzuri, kusema kweli Album hii ya MAUA, sijisifii lakini nasema baadhi ya wakongwe wajihadhari kwani moto wa Album hii sio wa Kitoto..." alisema Beatrice.



Beatrice amesemakuwa Video ya Album hiyo ndio iko jikoni inatengenezwa chini ya kambuni iitwayo kwetu studio ambapo album hiyo inabeba jumla ya nyimbo Nane. ikiwa ni pamoja na 1. Maua, 2. Roho Yangu 3. Ole Wako 4. Acha Kuloga 5.Shamesha Vavae 6. Yupo Mungu 7. Niseme na Yesu na wa 8. Maua no.2
"... Kusema ukweli nawaomba watanzania watarajie kupata Video bora ambazo ni tofauti na zile zilizozoeleka, hizi zitakuwa nzuri na zinazoendana na Ujumbe wa nyimbo husika..." alimalizia Beatrice.
akasema pia kwa yeyote anayetaka kuupata wimbo wa Maua kupitia Whatsap anaweza kutumia namba hii kuupata. 0757 890 451

Friday, June 3, 2016

TB JOSHUA ATOA MSAADA KWA TANZANIA... AMKABIDHI MAMA MAGUFULI...

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli amemshukuru nabii TB Joshua wa Nigeria kwa msaada alioutoa kwa Tanzania baada ya kuongea nae na kumueleza maono yake ya kusaidia wazee na watu wenye ulemavu..
Mama Janeth amesema Namshukuru kwa msaada huu mkubwa aliotuwezesha katika kambi hii ya Wazee, nilipoongea nae nilimueleza maono yangu kwa ajili ya huduma hii ninayofanya ya kuhudumia Wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza
Niliongea nae akasema ataniunga mkono na kama mnavyoona hapa leo yeye mwenyewe ametuma mwakilishi wake amenunua vyakula, namshukuru Nabii TB Joshua kwa kutoa, amekua akitoa misaada bila kujali itikadi za dini wala nchi… Mungu ambariki sana‘ Aliongea Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli

Tuesday, May 31, 2016

CHANZO CHA MATESO YA BENARD MWINJE IKO TAYARI... SOMA HAPA...


Benard Peter Mwinje
Mwimbaji wa nyimbo za injili na Mwalimu wa Kwaya Benard Peter Mwinje ameliambia Jicho Wazi kuwa tayari amekamilisha kupika Album yake yenye jumla ya nyibi Nane( 8)
Album hiyo iliyobeba jina la CHANZO CHA MATEZO, itaanza kupatikana mitaani hivi karibuni kwani kila kitu kiko tayari.
"... kusema kweli namshukuru Mungu kwani nimemaliza Kuandaa album yangu ambayo ina kwenda kwa jina la Chanzo cha mateso, wengi walidhani ntafeli lakini kwauwezo wa Mungu nimemaliza na hivi karibuni ntaaza kuisambaza kwani kama unavyoona hii hapa ndio kava lake ambalo nimetengeneza na Kampuni ya MO Design..." Alisema Mwinje.
akaongeza kuwa ataanza kuuza Audio tu peke yake ili apate pesa ya kuongezea katika maandalizi aliyonayo ya kufanya Video. Mwinje pia aliweka wazi kuwa yuko tayari kupokea mialiko mbalimbali kwani anachokifanya ni huduma ambayo iko ndani yake na kazi ambayo ametumwa na Mungu wake.
Nyimbo ambazo zinpo katika Album hii ya Chanzo Cha Mateso ni pamoja na. Chanza cha Mateso, Ukiwa na Raha, Mbinguni, Dhahabu, Duniani, Kwa neema, Nijifiche wapi pamoja na Mungu Wangu.

CHANGAMOTO: NI COVER IPI KATI YA HIZI INAFAA KUTUMIWA NA MWIMBAJI AGNESS NKUNGWE?.. USHAURI WAKO...


Mwimbaji Agness Nkungwe
Hakuna kazi duniani inayokosa changamoto, unaweza ukafanya kitu katika maisha wewe ukaona uko sahihi lakini jicho la pembeni likaona unachapia,
Hata katika kazi hizi za kudesign Cover na posters, watu wanakutana na changamoto nyingi zingine ukiziangalia zinakuwa hazina msingi lakini ilimradi tu nichangamoto imetoke.
katika kulichunguza hili, Jicho Wazi tulitazama hizi Cd Cover zilizotengenezwa na MO Design na tukaambiwa kuwa moja kati ya hizi ndio ilikuwa sahihi lakini mwenyewe alivyozitazama akaikataa na kisha kuomba mabdadiliko.


Sasa Jicho Wazi tungependa kuwaomba watazamaji na ninyi mjaribu kuzitazama hizi Cd Cover za Mutumishi na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Agness Nkungwe kisha mtuambie ni ipi kati ya hizi mbili ambayo inafaa kutumiwa na huyu mtumishi. Agness Nkungwe.
Isiwe changamoto zingine zinaletwa tu na ushauri wa watu wengi na kukufanya wewe mwenyewe ushindwe kafanya maamuzi.

Thursday, May 26, 2016

HUDUMA YA MAACHILIO... UKOMBOZI NI HAKI YAKO... JUMAPI HII...



Jumapili hii Katika Viwanja vya Sifa zamani kama Viwanja vya Fisi, kutakuwa na HUDUMA YA MAACHILIO Itakayojulikana kama UKOMBOZI NI HAKI YAKO.... ibada hizi zitakuwa chini ya Apostle Paul Kaisi na Nabii Debora Kaisi... Hivyo unaombwa kufika bila kukosa ili ukutane na Mwisho, Huzuni, vilio visivyoisha katika ndoa yako, Kazi zako, Biashara zako na Mwengine Mengi.

Huduma Hii itakuwa kama ifuatavyo, IBADA YA KWANZA ITAANZA SAA1:00 Mpaka SAA 3:00 ASUBUHI... Wakati IBADA YA PILI ITAANZA SAA4:00 Mpaka SAA 7:30 MCHANA.

Njoo ukutane na Watumishi wa Mungu ili Ukombozi wako utimie... KUMILIKI NA KUTAWALA NI HAKI YAKO.

Wednesday, May 25, 2016

ALFREDY FUNDA NA UMELIBEBA KUSUDI... HII NI MPYA KABISA...


Mwimbaji wa nyimbo za Injili lfred Funda

Huduma na Machozi Futa Machozi LIBEBE KUSUDI lako ukilibeba kusudi lazima wachawi wakutege komaa mwanangu mlilie Mungu maana anakusudi LA kukuleta duniani usishindane na mpumbavu atakuvunjia kusudi lako .....komaa

Haya ni maneno aliyoyaandika leo katika ukurasa wake wa Facebook Mwimbaji huyu wa nyimbo za injili Alfred Funda na ambaye anatamba kwa sasa na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la UMELIBEBA KUSUDI, kibao kilichotengenezwa katika Studio za Sandtone Records chini ya Producer Benja. wimbo huu ni katika mtiririko wa nyimbo zake nyingi ambazo tayari ameshaziandaa kwa ajili ya album yake.

Alfred Funda anaendelea kufanya vizuri katika wito wake na katika kulibeba Kusudi lake, ukilinganisha na huko aliko tokea ambapoa alikuwa anamwimbia Mungu kweli lakini katika mtindo wa Hip hop Gospel, hakuna aliyefikiria kuwa Funda ana sauti nzuri katika kuimba, na kama huamini basi utafute wimbo wake mpya huu ambao unatamba maredioni utaamini nikisemacho, kama hujaupata basi piga simu katika vituo vya redio wataucheza utajihakikishia niksemacho.